Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez anaonekana kuwa amebadili mawazo yake na kuamua kubaki na klabu hiyo .
Kwa
mujibu wa taarifa iliyonukuliwa toka kwa mwandishi wa habari aliye
karibu na Suarez Martin Chaquero Suarez amemhakikishia mwandishi huyo
kuwa ameamua kubaki ndani ya klabu hiyo ambapo ameeleza sababu yake
kubwa ya kubadili mawazo ni imani kubwa na upendo toka kwa mashabiki wa
klabu hiyo kuelekea kwake katika kipindi chote hiki.
Suarez
amesema kuwa mashabiki wa The Kops wamemuonyesha iamni kubwa ambayo
hana njia nyingine ya kuilipa zaidi ya kubaki ndani ya klabu hiyo.
Kwa
muda mrefu katika kipindi hiki ambapo dirisha la usajili liko wazi Luis
Suarez amekuwa akielezea azma yake ya kutaka kuondoka ndani ya
Liverpool sababu yake kubwa ikiwa kutaka kucheza Ligi ya Mabingwa barani
ulaya .
Klabu ya Arsenal ilipeleka ofa mbili za kumnunua mshambuliaji huyo lakini Liverpool ilizikataa ofa zote .
Kocha
wa Liverpool Brendan Rogers mwanzoni mwa wiki iliyopita alimpa Suarez
adhabu ya kufanya mazoezi mwenyewe kwa kuikosea heshima klabi hiyo baada
ya kufanya mazungumzo na waandishi wa habari na kuwaambia kuwa
Liverpool ilimuahidi kuwa ingemruhusu aondoke .
Kwa
mujibu wa mwandishi huyo Martin Chaquero Suarez amesema kuwa kuna
uwezekano way yeye kuongeza mkataba ambao utamfanya aendelee kuwa na
Liverpool kwa muda mrefu zaidi.
Hata
hivyo mshambuliaji huyo bado amegoma kuwaomba wachezaji wenzie msamaha
kama alivyoamriwa na kocha wake kwa kitendo cha kuwakosea heshima kwa
kuzungumza na vyombo vya habari.
0 comments:
Post a Comment