HISTORIA YA KANISA KATOLIKI NA MWINGILIANO WA FREEMASON KATIKA KULIBOMOA

Kwa
uchache kanisa la Roman Catholic ni kanisa la Roma, kama
linavyojulikana, kanisa la Roma.Roma ni mji mashuhuri uliopo Italia. Mji
wa Roma una historia ndefu katika dunia na ni mji uliotabiriwa na Mungu
pia.
Dunia
yetu imewahi kushuhudia ikitawaliwa na serikali moja katika awamu nne.
Awamu ya kwanza ilikuwa ni serikali ya dunia iliyopewa jina la Babeli.
Rais au mfalme wakwanza katika serikali hiyo alikuwa ni Nimrodi
akifuatiwa na Nebukadneza pamoja na marais waliomfuata. Asili ya
serikali hii ni mnara wa Babeli uliojengwa na mfalme wa kwanza wa
Babeli, rais Nimrodi. Eneo la sasa yalipokuwa makao makuu ya serikali ya
dunia awamu ya kwanza ni Iraqi.
Awamu
ya pili ya serikali ya dunia iliitwa Mede/Uajemi ambapo mmoja wa marais
wa serikali hii aliitwa Dario.Eneo la sasa yalipokuwa makao makuu ya
serikali hii ni Iran ya leo. Awamu ya tatu ya serikali ya dunia iliitwa
serikali ya Uyunani au Greece government. Mmoja wa marais mashuhuri
katika serikali hii alikuwa ni Alexander mkuu (Alexander the Great).
Awamu ya nne ya serikali ya dunia iliitwa‘Roman Empire’ au himaya ya
Roma. Mmoja wa marais wa serikali hii alikuwa ni Constantine. Serikali
hii ndiyo iliyotawala kwa muda mrefu kuliko serikali zote
zilizoitangulia.
Wakati
serikali hizo zinatawala dunia, dini ya kweli ilikuwa haijatikiswa hadi
serikali ya Roma ilipoanza kutawala. Je, dini ya freemasons ilianza
lini? Ukiondoa dini aliyoianzisha Mungu katika bustani ya Edeni, dini ya
freemasons ndiyo dini iliyoanza siku nyingi kuliko dini nyingine.Dini
hii ilianzishwa pia kwenye bustani ya Eden mwanzilishi wake akiwa ni
Shetani. Alimtumia Kaini anayejulikana kwa freemasons wa leo kama ‘first
freemason’ yaani mjenzi huru wa kwanza.
Hatimaye
rais Constantine kwa nusu aliamua kuachana na ibada za kipagani na
kujiunga na Ukristo. Hii ilikuwa ni kutimizwa kwa andiko la 2
Wathesalonike 2:3,4 maana ulikuwa ni ukengeufu wa kanisa la mitume
sehemu ya kwanza uliopelekea kuanzishwa kwa dini iliyochanganya ukweli
na uongo. Kwa nini dini hii ilisubiri hadi awamu ya nne ya serikali ya
dunia? Pengine nizungumzie kidogo maana ya namba nne kama inavyotumiwa
na Mungu. Namba nne sio namba maalumu kwa freemasons lakini ni muhimu
sana kwa Mungu. Namba nne inamaanisha kukomaa kwa mavuno na kuvunwa.
Tazama hapa: “Akawaambia ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu
aliyemwaga mbegu juu ya nchi…..Maana nchi huzaa yenyewe, kwanza jani, tena(pili)suke, kisha(tatu),ngano pevu katika suke. Hata (nne)matunda yakiiva
mara aupeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika” Marko 4:26 –kwenye
mabano ni ufafanuzi wa mwandishi. Hizo ni hatua nne kufika kuvunwa kwa
mbegu njema. Vipi habari ya mbegu mbaya? “Lakini kila mmoja hujaribiwa(kwanza)kwatamaa yake mwenyewe. Halafuile tamaa ikisha kuchukua mimba(pili), huzaa dhambi (tatu),na ile dhambi ikiisha kukomaa, huzaa mauti(nne)”Yakobo
1:14,15. Unaweza pia kujua ni kwa nini waisraeli walitumia miaka 40
(4x10) kutoka Misri hadi Kanaani; kwa nini Yesu, Musa walifunga kwa siku
40 (4x10). Kumbuka kwamba namba 10 kwa Mungu inawakilisha ‘ukamilifu wa
Mungu’ na namba 7 inawakilisha ‘utimilifu wa Mungu’.Kuna tofauti kati
ya ‘ukamilifu’ – ‘perfection’ na ‘utimilifu’ – ‘fulness’.Kitu kinaweza
kuwa ‘timilifu’ lakini kisiwe ‘kamilifu’ lakini kitu hakiwezi kuwa
‘kamilifu’ bila ya kuwa ‘timilifu’.
Kwa mfano mapigo 7 ni utimilifu wa ghabu ya Mungu lakini ukamilifu wa
hukumu yake utafikiwa wakati Shetani, dhambi na wadhambi
watakapoangamizwa motoni. Mungu alitoa amri 10 kwa wanadamu ikimaanisha
kwamba amri hizo zinawakilisha tabia ya Mungu ambayo ni ‘kamilifu’.
Lakini pia tunasoma “….Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima na ‘ukamilifu’ wa uzuri” kisha anaanza kutaja ni kwa namna gani alikuwa ‘mkamilifu’
wa uzuri akisema “1)Akiki, 2)Yakuti manjano, 3)Almasi, 4)zabarajadi,
5)shohamu, 6)Yaspi, 7)yakuti samawi, 8)zumaridi, 9)baharamani na
10)dhahabu. Lusifa alikuwa‘mkamilifu wa uzuri’ kutokana na kuvikwa aina 10 za madini ya thamani kubwa. Mungu ni‘mkamilifu’ kutokana na kuwa na tabia inayoelezewa kwenye amri 10katika Kutoka 20:4-17. Je wewe ni mkamilifu wa tabia kama ya Mungu kwa kuzitunza amri 10? Tafakari!
FREEMASONS NA FAMILIA 13 ZA ILUMINATI

Ni kwa namna gani Kristo alijitenga? E. White anaendelea kusema: “Pharisees and Sadducees were alike silenced. Jesus summoned His disciples, and prepared to leave the temple,
not as one defeated and forced from the presence of his adversaries,
but as one whose work was accomplished. He retired a victor from the
contest”. {DA 620.2}
‘Mafarisayo
na masadukayo walinyamazishwa. Yesu aliwakusanya wanafunzi wake, na
akawaandaa kuliacha hekalu, sio kama aliyeshindwa na kulazimishwa
kuondoka kwa maadui zake, bali kama ambaye kazi yake ilikuwa
imekamilika. Alikuwa ni mshindi katika mashindano”. {DA 620.2}
Biblia
inasema kwamba Yesu alijitahidi kupingana na mafarisayo na masadukayo
akiwa ndani ya mfumo wa dini ya kiyahudi na sasa alikuwa amefikia mwisho
wa upinzani wake na akaamua kujitenga moja kwa moja na mfumo wa dini
hiyo ili awafundishe vizuri wanafunzi wake ambao walikuwa tayari
kukubali mafundisho safi. E.G. White anasema:"
Hitherto He had called the temple His Father's house; but now, as the
Son of God should pass out from those walls, God's presence would be
withdrawn forever from the temple built to His glory. Henceforth its
ceremonies would be meaningless, its services a mockery. {DA 620.4}Hatimaye
Yesu na wanafunzi wake walijitenga na hekalu lililokuwa mpendwa wao.
Lakini kwa sababu viongozi wa hekalu walikataa kufuata mafundisho ya
neno la Mungu peke yake, Mwana wa Mungu hakuona sababu ya kuendelea
kubaki ndani ya hekalu ingawa “Alikuwa akiliita hekalu kuwa ni nyumba ya
Baba yake; lakini sasa, kama Mwana wa Mungu ambavyo akipita kutoka
katika kuta hizo, uwepo wa Mungu ungeondolewa milele usionekane ndani ya
hekalu lililojengwa kwa utukufu Wake. Hivyo sherehe zilizofanyika ndani
ya hekalu hazikuwa na maana, huduma zake zikawa dhihaka”. {DA 620.4}.
Hivyo ndivyo alivyofanya Martin Luther na wafuasi wake.
Baada
ya kifo cha Martin Luther, wafuasi wake waliendelea katika kufanya
matengenezo. Hata hivyo kwa sababu freemasons hawakati tamaa,
matengenezo yalikoma na kuanza kurudi nyuma taratibu ambapo leo hii wale
wanaoitwa ‘Walutheri’ wameungana tena na mfumo ambao mwanzilishi wao,
Martin Luther, aliuiita ‘mfumo mchafu’.
Wakati
matengenezo yanaendelea, ulikuwa ni wakati wa kutimizwa kwa unabii wa
siku 1260 sawa na miaka 1260 kama ilivyotabiriwa na nabii Yohana. Wakati
huo kulianzishwa matengenezo mengi na kupelekea kuanzishwa kwa mifumo
mingine ya makanisa. Baadhi ya makanisa yaliyoanzishwa yalikuwa haya:
Anglican:
Lilianzishwa huko England na mfalme wa Uingereza ili kupinga kanisa la
Roma. Kiongozi mkuu wa kanisa hilo ni Malkia wa Uingereza. Hata hivyo
wachunguzi wa dini ya freemasons wanasema kwamba familia ya Malkia ni
familia mojawapo kati ya familia 13 za waumini wa Freemasons.
Presbyterian:
Mwanzilishi ni John Calvin mwaka 1509 – 1564 na John Knox 1505 – 1572.
Kanisa hili lilijitenga na Roma likiwa na motto “Chunguza maandiko”
maana liliona kwamba kanisa la Roma linakwenda kinyume na maandiko. Hata
hivyo wafuasi wa John Calvin na John Knox wameshindwa kufikia malengo
ya kuyachunguza maandiko na kufuata kile asemacho Mungu na badala yake
wamekubali kurudi walikotoka!
MENNONITE:
Lilizaliwa rasmi mwaka 1525 – 1530 na Conrad Grebel na wenzake akiwemo
Zwingli Ulrich aliyetofautiana na Martin Luther juu ya somo la pasaka.
Hawa walikataa ubatizo wa Roma wa kunyunyizia maji na jina jingine
wanaitwa “Meno Knights” majina ambayo yanafanana na vikundi vya
Freemason kama vile “The knights of Eulogia”(Skull and Bones), “The
knights of Malta”. Ingawa lengo la Zwingli Ulrich lilikuwa zuri, baada
ya kifo chake wafuasi wake walikubali kuingiliwa na freemasons na hivyo
kushindwa kufikia lengo lililokusudiwa.
LUTHERAN:
Mwanzilishi ni Martin Luther mwaka 1517. Alikuwa ni Mjerumani
aliyesomea ukasisi wa kanisa la Roma na mwaka 1511 akapata Phd katika
chuo kikuu cha Wattenberg. Alipingana na kanisa lake la Roma na kuandika
sababu 95 zinazopinga mafundisho ya Roma ndipo akajitenga na Roma na
hivyo wafuasi wake wakaendelea kutumia jina la Lutheran, yaani wafuasi
wa Luther. Wafuasi wa Luther hawakuendelea mbele na sasa wamerudi kwenye
makosa aliyokuwa akiyapinga Luther. Je, Lutheran wa leo wanafuata kweli
nyayo za Martin Luther? Au wametekwa kwa matumizi ya njama ya
“Following Gurus”yaani kufuata kila wasemacho viongozi? Tafakari!
Moravian:
Mwanzilishi ni John Huss aliyezaliwa mwaka 1366 na kuchomwa moto na
papa hadi kufa mwaka 1416 baada ya kulipinga kanisa la Roma. Wafuasi
wake hadi leo wanaitwa kanisa la Moravian. Kwa bahati mbaya wafuasi wa
John Huss hawakuendelea kufanya matengezo ili kusonga mbele zaidi ya
Huss na kibaya zaidi ni kwamba wanarudi nyuma badala ya kusonga mbele.
Leo Huss akifufuka atashangaa kuona jinsi wafuasi wake walivyoacha
kanuni alizozianzisha. Je, wamoravian wa leo wako tayari kuchomwa moto
kwa kutetea ukweli kama John Huss? Tafakari!
Baptist:
Ni kanisa lililoanzishwa na wafuasi wa Martin Luther ambao walijitenga
na Lutheran mwaka 1600 huko Uholanzi na Uingereza baada ya kuona kwamba
wafuasi wenzao wameacha kanuni alizoziweka Martin Luther. Hata hivyo
kanisa la Baptist la leo haliendeleza jitihada za Luther na sasa badala
ya kusonga mbele linapiga ‘marktime’ likiwa limegeuka nyuma.
Salvation Army (Jeshi la Wokovu):
Mwanzilishi ni Booth mwaka 1878. Kanisa hili lilianzishwa na wafuasi wa
freemasons kwa lengo la kuchafua matengenezo ya kweli. Kumbuka kwamba
Shetani hutumia fursa inayotolewa na Mungu akiwa na lengo la kuwafanya
watu washindwe kujua kipi ni cha kweli na kipi sio. Katika kila
matengenezo ya kweli, pamekuwepo na matengenezo bandia.
Marmon church:
Mwanzilishi ni Joseph Smith (1805 – 1844). Kanisa hili linajulikana pia
kama The church of Jesus Christ of later day saints. Kanisa la Mormon
lilianzishwa na wafuasi wa freemason wakiwa na lengo la kuchafua
matengenezo ya kweli. Mitt Romney ni muumini wa kanisa la Mormon.
Methodist: Kiongozi Mwanzilishi ni John Wesley. Lilianzishwa na watu 17 wa familia moja
mwaka 1738 likiwa na lengo la kupinga mafundisho ya freemasons. Kanisa
hilo halijakamilisha lengo la matengenezo kutokana na ukweli kwamba
wafuasi wake hawana mwamko aliokuwa nao John Wesley.
Watch Tower:
Mwanzilishi ni Charles T. Russel 1852 – 1916 na mwenzake J. Lutheford
1869 – 1942. Baba yake Charles T. Russel alikuwa ni mchungaji wa
Prebyterian. Mnamo mwaka 1932 huko Marekani jina la kanisa hilo
lilibadilishwa na kuitwa Mashahidi wa Yehova. Markus Mpangala ameelezea
kwa kirefu chanzo cha dhehebu hili akiainisha kwamba waanzilishi
walikuwa ni Freemasons kutoka kwenye familia ya Illuminati inayoitwa
Russel illuminati bloodline ambayo nimeshaielezea kwenye makala
zilizopita.
Brethen Assemblies:
Mwanzilishi ni ndg. Dabi 1800 – 1882 ambaye alikuwa ni muumini wa
Anglican na akajitenga na kanisa hilo na kuanzisha kanisa lake. Dabi
aliamua kujitenga na Anglican kutokana na kanisa hilo kutawaliwa na
familia ya freemasons.
Makanisa ya Kipentekoste au kilokole:
Ni makanisa yaliyoanzishwa miaka ya hivi karibuni. Makanisa haya
yalianzishwa huko Kansas City Marekani mwaka 1901kwa lengo la kupata
nguvu ya kile kinachoaminiwa kuwa roho mtakatifu. Je, unajua uhusiano
uliopo kati ya muziki wa‘rap’ au ‘kufoka’ na uvuvio wa kunena kwa lugha
kutoka kwa kile kinachoaminiwa kuwa ni nguvu za roho mtakatifu wakati
waumini wa kilokole wanapokuwa wakiomba? Kumbuka kwamba Muziki wa rap
ulianzia huko Kansas City Marekani, mahali ambako makanisa ya
kipentekoste yalianzishwa. Panapo majaaliwa, nitakuwa na makala ndefu
kuhusu asili, lengo na nguvu inayoonekana kwa viongozi wa makanisa ya
kilokole kama akina T.B Joshua wa SCOAN la huko Nigeria. Kwa wakati huu
nasema,‘Soma Biblia na Tafakari’!
Gospel terbenacle: Mwanzilishi ni Pastor A.B. Simpson mwaka 1881 akitokea Presybiterian.
Christian Churches: Mwanzilishi ni Thomas Chapel mwaka 1807 akitokea Presybiterian.
Seventh –Day Advetist Church:
Mwaka 1844 baada ya kutokurejea kwa Yesu duniani kama ilivyohubiriwa na
muhubiri mashuhuri aitwaye William Miller, watu wengi walivunjika moyo
isipokuwa watu 50 tu ndio walioendelea kujifunza Biblia miongoni mwao
akiwa ni Ellen G. White. Watu hao waliendelea kuchunguza makosa
yaliyofanywa na William Miller maana wao pia waliamini juu ya marejeo ya
Yesu tarehe 22/10/1844. Hatimaye mwaka 1863 kanisa hilo likapewa jina
la Seventh –Day Adventists Church huku likiwa na motto au kauli mbiu ya
“Amri za Mungu na imani ya Yesu na Ujumbe wa malaika watatu” na baadaye
kanisa hilo likawa chini ya rais
wa General Conference ya SDA makao makuu yake yakiwa huko Marekani.
Rais huyo ndiye kiongozi (kichwa) mkuu wa kanisa hilo duniani na
huchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Wakati viongozi wa kanisa
walipokutana ili kujadili mambo ya kanisa, palikuwa na
‘Mwenyekiti’(Chairman of General Conference) ambaye aliongoza kikao hadi
mwisho. Baada ya kikao kumalizika, mwenyekiti huyo alimaliza muda na
kazi yake. Hata hivyo kulitokea mabadiliko kutoka mwenyekiti wa baraza kuu hadi na rais wa kanisa ulimwenguni. Kila baada ya miaka mitano hufanyika uchaguzi wa kumpata rais
wa kanisa hilo. Tofauti na makanisa mengine, kanisa hili linaabudu siku
ya Jumamosi wakati makanisa mengine yanaabudu siku ya jumapili. Sasa
hivi kuna makanisa mengi ya SDA ambayo yametoka ndani ya kanisa la
‘General conference of Seventh-Day Adventists’(GCSDA) kwa madai kwamba
kanisa hilo limeingiliwa na freemasons. Wengi wa waumini wa SDA
waliojitenga na GCSDA wanasema kwamba walikuwa wakipinga‘protest’
mafundisho machafu huku wakiendelea kuwa ndani ya GCSDA lakini
hawakuweza kuleta mabadiliko yoyote maana hali ilikuwa inazidi kuwa
mbaya. Hatimaye waumini hao waliamua kufuata nyayo za akina Luther za
kujitenga na sasa wanafanya ‘reformation’ au ‘matengenezo’ hatua kwa
hatua maana walitoka na mafundisho machafu ambayo waliyapokea kama kweli
wakiwa ndani ya GCSDA.Waumini hao wanadai kwamba walijitenga na GCSDA
kwa sababu
Je, madai hayo ni kweli? Tafakari!
Msingi
wa kanisa la SDA au ‘Wasabato’ kama inavyojulikana kwa wengi,kuabudu
siku ya jumamosi, ni kile kilichoandikwa na Mungu wakati wa uumbaji,
kwamba aliumba kwa siku 6 na siku ya 7 akastarehe, akaibariki na
akapumzika kisha akawaambia waisraeli: “Ikumbuke siku ya Sabatouitakase….” Kutoka 20:8.
Kutokana
na kazi ya chama cha Priory de Sion kwa kuingiza mafundisho machafu
ndani ya imani safi, kulitokea utitiri wa makanisa mengi ambayo yanadai
kupinga uchafu huo. Hata hivyo wengi wa waumini wa madhehebu hayo ama
hawajui asili ya dhehebu lao au hawajui asili ya kile wanachokiabudu.
Wengi wamefundishwa na waalimu wa dini na kuwaamini bila hata ya kutaka
kuhakikisha kwa akili zao kile wanachofundhishwa. Mungu ametoa nafasi ya
kufahamu ukweli kwa kila mmoja wetu bila ya kutegemea viongozi wa dini.
Umewahi kufikiri kwamba kama ungekuwa unaishi duniani wewe peke yako,
ungemtegemea nani? Tafakari!
0 comments:
Post a Comment