abdalah
alikuwa na mwanamke mwingine wakifanya mapenzi hakuonyesha mshtuko yeye
aliendelea na tendo nilibaki nimesimama pale mlangoni natetemeka na meno
yakigongana kwa hasira Yule mwanamke baada ya kuona siondoki alichokifanya
akazidisha sauti ya mahaba
!!iiiihiii abdalah
wangu nipe mambo wewe ndo mwanaume unayejua kunifikisha,
Huku akikata mauno na
kugeuka kila staili ili kuonyesha yeye alikuwa fundi nilishindwa kuvumilia
niliondoka eneo lile na kurudi nyumbani nakumbuka siku hiyo nililia sana kama
mtu aliyefiwa na kuondokewa na mtu muhimu katika maisha yake sikupenda
kuwashirikisha marafiki zangu, katika matatizo yangu,
nililia sana hadi macho
yakavimba usiku ulivyoingia nilipanda kitandani na kulala asubuhi nilipoamka
kichwa kilikuwa kinaniuma sana nikaangalia simu yangu ya mkononi kama abdalah
alinitafuta kwa kunipigia au kunitumia sms lakini haikuwa hivyo,
nilizidi kuumia
kwa sababu nilikuwa nampenda na nilikuwa nipo tayari kumsamehe endapo
angeniomba msamaha baada ya kupita wiki moja bila ya kunitafuta ilibidi
nimpigie simu ‘’
!!hallow mpenzi wangu
abdalah,
!!alijibu mpenzi!!!
nani mpenzi wako?
!! abdalah jamani
nimekusamehe najua ulipitiwa ndio maana ukanisaliti naomba turudishe mapenzi
yetu kama zamani,
!!unisamehe we vipi
kwani mimi nimefanya kosa gani? Tena usiniambie hizo habari kwa sababu
uliniudhi sana kwa nini umekuja nyumbani kwangu bila taarifa?
!!we abdalah unasemaje
yaani umenisaliti alafu bado unaongea lugha mbovu nimekoma kuanzia leo hutoona
nimekutafuta asante sana.
Nilikata simu nililia
sana siku hiyo nikafanya maamuzi nikasema sitompigia tena simu baada ya muda
nikaanza kuzoea maisha ya kuwa mwenyewe miezi michache iliyofuata nikachaguliwa
kujiunga na chuo kikuu sikupenda kukaa katika hostel za chuo nilitafuta chumba
nje ya hostel na kupanga
nilianza mwaka wa kwanza nikiwa sina mpenzi kwa
kipindi hicho wanafunzi waliopo chuo mwaka wa pili hadi wa tatu wanapowaona tu
wanafunzi wapya wa mwaka wa kwanza kwa wanaume wasiotulia kazi yao kubwa ni
kuwatongoza hao wasichana,
na wanapowapata hujiita vidume kwa kulala na wasichana wengi wa
chuo ndivyo ilivyotokea kwa upande wangu kwani kuna kijana mmoja
aitwae aron john alikuwa ni mtoto wa kitajiri alipatiwa pesa za kutosha na
wazazi wake kiasi kwamba hata wanafunzi wa kike walio na tamaa walikuwa
wakimshobokea,
na kwa kuwa yeye anapenda kuonekana na idadi kubwa ya wanawake
alifanya nao mapenzi na kuwapatia pesa nilipo
ingia tu pale chuo stori nyingi zilimzungumzia yeye sikupenda tabia aliyokuwa
anaifanya siku moja wakati napitapita katika maeneo ya chuo nilikutana na aron
pale pale alinisimamisha
“ dada samahani nina
mazungumzo na wewe’
huku mkono wake ukiwa katika bega langu ili kunizuia
nisipite,
‘nikamjibu…. ‘embu
niache kwani lazima unishike’ huku nikiwa nimekunja uso wangu,
‘akanijibu…. ‘kwa nini
umekasirika kiasi hicho kwani nimekukosea? Nahitaji nipate muda wa kuongea na
wewe,
Nikamjibu….;no sina
muda wa kuongea na wewe jaribu kwengine, nikaondoka zangu nikamuacha hapo akiwa
amesimama hakuamini kilichotokea hakuchoka aliendelea kunisumbua kila mara
tulipo kutana na msimamo wangu ukawa hivyo sikutaka kumpa nafasi ya kuongea na
mimi ..........
ITAENDELEA .....
0 comments:
Post a Comment