DR LOVE....
alikuwa ni kijana mpole tena mwenye kuheshimika na kila mtu alifanya kazi yakushauri wenye matatizo ya kimapenzi na hata kutoa elimu juu ya kuimarisha
upendo kwa walio kwenye mahusiano ya kimapenzi aliandika vitabu vya story za
mahaba maneno yaliyoandikwa yalikuwa yanahisia kila msichana aliyesoma
alitamani sana kuwa naye kimapenzi kwani maneno yake yalikuwa yakujali yakuthamini
na ya upendo tatizo kubwa alilokuwa nalo alishindwa kuishi na msichana yeyote
ambaye aliingia naye kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa sababu yale
aliyoyaandika na kuyajua alishindwa kuyatumia kwa mpenzi wake hakumjali wala
alikuwa hawezi kutamka maneno mazuri ya mahaba pindi anapokuwa na mpenz
wake.........
UNATAKA KUJUA UNDANI WA MAISHA YA DR LOVE? FUATILIA
SEHEMU YA KWANZA (1)
Dr love kwa jina lake halisi aliitwa joel ludovic siku zote alipenda kuishi kwa haki
bila kuonewa alipenda kuwaheshimu watu warika zote awe maskini au tajiri pia
katika maisha yake ya nyumbani au shuleni alipenda sana usuluhishi watu
walipokuwa wanagombana yeye alitoa ushauri na watu pia walipatana, ‘’ kwa jambo
hilo wanafunzi wengi walipenda kuwa na karibu naye walimwamini na kumwambia
siri zao na hata siku moja hazikuwahi kuvuja ama kuzisikia kwa mtu mwingine
ilimpa urahisi wa kusuluhisha matatizo ya watu kwa sababu alipata maelezo
kutoka pande zote mbili pia alipata uzoefu kupitia matatizo ya watu aliendelea
hivyo hadi alipomaliza elimu yake ya secondari na kuingia elimu ya juu chuo
kikuu hata alipofika huko aliendelea na kazi yake ile ile ya kuwashauri watu
baadhi ya wasichana ambao hawakuwa na mazoea naye walimwita Malaya kwa sababu
mara nyingi alikuwa karibu sana na wasichana, kwa hilo walihisi ana mahusiano
nao ya kimapenzi lakini haikuwa hivyo, ‘bado alikuwa hajaona chaguo lake, ‘’aliendelea
kupata umarufu na kujulikana wengi walipenda kumwita dr love….
Siku moja joel alikuwa anatoka chuo, akiwa njiani anatembea kuelekea kituo cha basi akaangusha
pochi, ‘’ila hakugundua akapanda Daladala kulikuwa na baadhi ya wanafunzi ambao alipanda
nao, muda wa kondakta kudai nauli ukafika akachukua nauli kwa wengine kufika
kwake kujisachi mfukoni akagundua kuwa hana pochi akajiuliza ameangushia wapi
hiyo pochi wakati akiendelea kufikiria kondakta akaropoka
‘’ebwanaaa vp mbona hutoi huo mshiko fanya fasta nakusubiri wewe
ikabidi amwambie kuwa hana hela amedondosha pochi yake,
konda kusikia hivyo akaanza kumtukana na kumwambia kama unataka amani toa hiyo nauli, hutoshuka salama nakwambia kama unataka kupasuka
uso wako usinipe hela yangu”
miongoni mwa wanafunzi aliopanda nao walikuwa
wasichana wawili angel na julieth waliyasikia maneno ya konda lakini wakakaa
kimya, hawa walikuwa marafiki waliopenda sana kuzoeana na joel ila walimwona kama
Malaya, kwa upande wa julieth alitamani sana kuwa naye kimapenzi ila alishindwa
amwanze vipi, angel akamnong’oneza julieth akamwambia leo joel atakoma hana
nauli, ‘julieth akamwambia lakini angel huoni kama hii ndo nafasi ya kujuana naye me namlipia nauli akamwita konda
samahani nauli ya huyu kaka hii hapa huku akiwa ameishika mkononi, konda
alipoiyona akamwambia joel ‘dume zima linalipiwa hiloooo, lakini joel hakupenda
ugomvi siku zote aliamini kwamba ukibishana na mjinga na wewe utakuwa mjinga
akamwambia julieth '
asante dada mungu akubariki samahani unaitwa nani? julieth
akageuka akamwambia
naitwa julieth ‘na pia usijali kaka kawaida tu’ huku akitoa
tabasamu zuri lenye dimpoz joel aliliona hilo naye pia akatabasam angel alikuwa
wakwanza kushuka akabaki julieth kuendelea na safari kila muda joel aliendelea kumtizama akajisemea
moyoni ‘’ila huyu dada ni mrembo sana amewazidi wasichana wengi pale chuoni
nilikuwa wapi kumwona huyu dada’’
kumwangalia kwake hadi julieth akaanza kujishtukia kituo kilichofuata
akashuka julieth akamuaga joel na kuondoka, ‘’joel alikuwa amepanga chumba
kimoja alivyofika anapoishi aliendelea
kumuwaza julieth alishindwa kuelewa kwa nini hali imemtokea, kesho yake
alivyofika chuo akajaribu kumtafuta lakini hakumpata ikabidi akakae kituoni na
kumsubiri alimsubiri sana lakini hakutokea siku iliyofuata alifanya hivyo hivyo
kila mtu aliyefika kituoni alimuuliza vp mbona kila siku unakaa hapa kituoni’’ hakuwajibu kitu, wengine walimtania kwamba
‘’ahaaa siku hizi unauza chenchi kwa makonda nini maana hutoki hapa’’ lakini
joel alicheka tu baada ya muda alikuwa amejiinamia na akapitiwa na usingizi pale pale alipokuwa amekaa kutokana na
mawazo aliyonayo kwa julieth akaanza kuota ndoto huku akimtaja kwa jina julieth
nakupenda sana kuna wanafunzi wawili walifika wakamkuta joel akiwa usingizini
mmoja wao akamfuta na kumgusa bega............
Katika familia ya julieth walizaliwa wawili akiwa
yeye na mdogo wake aliyeitwa deo wazazi wao walifariki kwa ajali ya gari enzi
za uhai wa mama yake julieth alikuwa akiamini sana imani za kishirikina
alipenda sana mwanae asome hadi elimu ya juu katika kipindi hicho alikuwa
ameingia kidato cha kwanza na alijua tu kuna kipindi kitafika atapata
vishawishi kutoka kwa wanaume njia aliyoigundua ni kwenda kwa mganga na kupewa dawa kwa ajili ya kumpaka sehemu za siri endapo atapata mpenzi na kufanya naye mapenzi ikiwa bado hawajaoana atapata
maumivu makali sehemu za siri siku zote ambazo atashiriki tendo hilo la ndoa mama yake akakubali na kuipokea ile dawa pasipo kufikiria madhara ambayo mwanae angeyapata alipofika
nyumbani akamuita julieth chumbani na kumpa masharti ya ile dawa akamwambia vua
nguo ili ampake julieth akakataa ikabidi mama yake atumie nguvu akafanikiwa
kumpaka ile dawa sehemu za siri na kumwambia
''mwanangu usije ukajaribu kufanya mapenzi na mwanaume yeyote hadi
hapo utakapofunga ndoa endapo utavunja masharti dawa hii itakutesa hutaweza kupata raha ya kufanya mapenzi kamwe,
julieth akakubali tangia siku hiyo hakujaribu kuingia kwenye mahusiano na mwanaume yeyote hadi
anafika elimu ya chuo kikuu hakuna mwanaume aliyeweza kumshawishi kimapenzi, uzuri
wake ulimfanya apate sana usumbufu kutoka kwa wanaume na kipindi hicho mdogo wake pia alikuwa darasa la sita.............................
Baada yakuonana na joel kwenye daladala na kuongea naye alitamani sana akifika chuo
aweze kuonana naye tena lakini siku iliyofuata alipoamka asubuhi mdogo wake deo alikuwa
anaumwa ikabidi asiende chuo ampeleke hospitali na siku hiyo joel alikaa kituoni kumsubiri ila siku ya pili alipokwenda chuo wakati anatoka na kuelekea kituo cha daladala akamkuta joel amelala kituoni baada ya
kumsogelea ili kumuamsha ile anamgusa tu joel alishtuka na kusimama wima na kujigonga katika nondo iliyoshikilia kituo alipata maumivu makali eneo la kichwani, alibaki anamwangalia tu julieth bila kuongea lolote huku akiwa ameweka mikono yake kichwani eneo aliloumia,
julieth akamwambia pole sana vipi mbona umelala kituoni?
akamwambia
nilikuwa nakusubiri wewe julieth,
‘unanisubiri mimi kwa nini?
Joel akapiga kelele kuonyesha kuumia ile sehemu aliyojigonga,
Julieth akamwambia vipi mbona hivyo?
akamwambia nimeumia sana pia nina maumivu makali kichwani,
Julieth akamsogelea na kumwambia wapi hapo kama vipi twende hospitali,
joel akaona hii ndo chance alipomsogelea tu akaanza kumkiss kama dakika moja,
‘ikabidi julieth amsukume na kumwambia vipi mbona umenikiss?
Joel akamwambia kwa sababu nakupenda nakuhitaji kuliko kitu chochote na mapenzi niliyonayo kwako ndo yamenifanya nikae hapa kituoni kukusubiri wewe
‘Julieth akamnasa kibao usoni na kumwambia sikupendi na wala sikuhitaji usijaribu kufanya huu mchezo siku nyingine akasimama ili aondoke wanafunzi waliokuwepo kituoni walimcheka sana joel………………..
ITAENDELEA
NINI KITATOKEA BAADA YA HAPO
0 comments:
Post a Comment