Connection

Services

Computer Maintanance

Computer Supply

Laptop Repair

Networking Installation



Learn more

Wednesday, 28 August 2013

Filled Under:

(LYRICS)

Share

NAY WA MITEGO NYIMBO -SALAM ZAO
(Verse1) 
Me ndio raisi wa manzese yule tozi kasanda 
Manzese mikono juu naiongoza kamanda 
Wanangu nyongeni ganja msiogope polisi 
Ila tu msile unga mtapoteza nafasi Me ndio gangster rapper na kiboko ya marapper
Wanaleta ushindani mwishoni wanatoka kapa 
Me natengeneza hela wao wananuka vikwapa 
Eyo mchovu wape salam kubum kubam Waambie watakufa nao mziki umebadilika 
Napenda mnavyonidisi wala hamnitishi
Walap diamond we si mtoto wa kigoma Mpe salam zitto kabwe mwambie afanye siasa 
Aachane na bongofleva huku atumtaki kabisa Maneno mengi 
propaganda hajui kutekeleza Kigoma allstars tayari kawatelekeza 
Naongea na ridhiwan eyi ridhiwan We si mtoto wa rais ridhiwan 
Mwambie dingi yako masela hawamuelewi 
Wamakonde wa mtwara hawataki tena korosho 
Wanataka gas si mtawauwa kwa mkong'oto 
Nani rafiki wa Lowasa peleka salam 2015 nataka agombee uraisi 
Nitamfanyia kampeni wananchi wampe nafasi 

(Chorus) 
We nenda wape salamu zao 
Waambie sina tatizo nao 
Wakivimba wapasuke 
Hizi salamu zifike kwao 
We nenda wape salamu zao 
Waambie sina tatizo nao 
Wakivimba wapasuke Hizi salamu zifike kwao 

(Verse2) 
Sina beef na polisi Mbunge wala raisi 
Hizi ni salam tu nataka tuishi peace 
Mkimaindi amna noma Sio muelewa kula kona 
Hizi salam toka bongo nataka zifike kenya Uganda 
hakuna matata najua ngoma inapenya 
Mambo vipi ccm mnasemaje chadema Cuf bado ngangari au tayari mshabuma 
Na salamu muhimu ziende kwa watu maalum 
Nani nimtume kuzimu afikishe salamu Kwa kanumba na ngwair 
Siku ya misiba yao kuna watu wamepigaa hela 
Wanamiliki magari wameota na vitambi Kwa hela za rambirambi 
Kwa majina nawajua mkizingua nawataja 
Msisitizie Na kanumba Baada ya yeye kufa Na bongo movie imekufa haiuzi kabisa 
Hizi salamu ziende kwa madam ritha na bongo star search 
Mshindi analipwa nini mbona kama magumashi 
Namuona walter chilambo kapigika kama zamani 
Haji ramadhani kachoka yupo kitaani Milion hamsini zao anazila nani 
Hacheni ubabaishaji wekeni mambo hadharani 
Tanzania bila uchafu kumbe inawezekana 
Yoo Jakaya mualike tena Obama Japo ujio wake kwa wengine ni lawama 
Walalahoi wenzangu mishe zao zinakwama 
Nani nimtume dodoma afikishe salamu bungeni 
Kuna wabunge vilaza bungeni wao wanalala tu 
Na wakiamka kila hoja ndio tu 
Kuna vilaza part two wao matusi na kulumbana tu 
Mawaziri vivuli wanakazi gani wana maana gani wana faida gani 
Wabunge viti maalumu wana kazi gani wana faida gani Mbona me sielewi 

 (Chorus) 
We nenda wape salamu zao 
Waambie sina tatizo nao 
Wakivimba wapasuke Hizi salamu zifike kwao 
We nenda wape salamu zao 
Waambie sina tatizo nao 
Wakivimba wapasuke Hizi salamu zifike kwao

0 comments:

Post a Comment

2014 © Movieism
RealMag theme by Templateism