LEO OLD TRAFFORD: NI MAN UNITED v LIVERPOOL!
>>KWA MOYES NA MAN UNITED, NI USHINDI AU WASHABIKI ‘WATAASI!’

Mvuto wa kwanza ni nini kitatokea leo
kwa Mabingwa wa England, Manchester United, ambao chini ya Meneja mpya
David Moyes, Juzi Jumapili walibamizwa Bao 4-1 na Mahasimu wao wa Jiji
la Manchester, Man City, Uwanja wa Etihad kwenye Mechi ya Ligi Kuu
England.
Mvuto wa pili ni Luis Suarez, Straika
‘Macheche’ wa Liverpool ambae leo hii ndio itakuwa Mechi yake ya kwanza
tu baada ya kumaliza Kifungo cha Mechi 10 alichopewa tangu Mwezi Aprili
kwa kumng’ata Meno Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic wakati wa Mechi ya
Liverpool na Chelsea.
+++++++++++++++++++++++++++
CAPITAL ONE CUP
RAUNDI YA TATU
RATIBA
Jumatano Septemba 25
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Birmingham v Swansea
Manchester United v Liverpool
Newcastle v Leeds
Tranmere v Stoke
[Saa 4 Usiku]
West Brom v Arsenal
+++++++++++++++++++++++++++
David Moyes: Ukicheza na Liverpool ni upinzani mkubwa!!
Hapo Jana, David Moyes, wakati wa
Mahojiano na Wanahabari, alisema: “Ukiwa Meneja kwa muda mrefu kama
nlivyokuwa mimi, Siku zote utapata mistuko. Nishapata mingi. Sina
wasiwasi itakuwepo mingine baadae. Hivi ndivyo Soka lilivyo. Huwezi
kukaa muda mrefu unafikiria hayo. Yamepita hayo, siwezi kufanya lolote
kuhusu hayo, tunasonga mbele. Tunaangalia Gemu ijayo na kujaribu
kushinda. Nina motisha kwa kila Gemu.”
Akiongelea Mechi hiyo ya Capital One Cup
dhidi ya Liverpool, Moyes amesema: “Ni Gemu muhimu kwetu. Tunataka
kujaribu kufanya vyema katika Vikombe vyote. Siku zote ni Gemu kubwa
ukicheza kwenye Vikombe. Ukicheza na Liverpool ni upinzani mkubwa.
Inaweza ikachukuliwa ni Gemu kubwa kwa sasa lakini mwishoni ni Mechi
kama nyingine tu.”
Kuhusu ile desturi ya kuchezesha
Chipukizi kwenye Mashindano haya ya Capital One Cup, Moyes alieleza:
“Kombe hili Siku zote limekuwa ni njia ya kujaribu na kuwapa nafasi
Vijana. Lakini inategemea Droo yenyewe na wakati mwingine unaweza
kufanya hivyo. Lakini hii ni Mechi kubwa iliyotoka kwenye Droo hiyo.”
Robbie Fowler: Luis Suarez nafasi ya mwisho kwake Liverpool!!

Fowler amesema: “Nadhani Suarez ataanza
katika Mechi hii kwa sababu mbili: kwanza anahitaji Mechi na bila ya
kuwepo kwa Philippe Coutinho alieumia ipo nafasi kwake. Ukweli ni kuwa
kama Liverpool haitamaliza katika 4 bora Msimu huu, Suarez ataondoka.”
Alipohojiwa kama hii ni nafasi ya mwisho
kwa Suarez kujirekebisha kwa tabia zake za utovu wa nidhamu, Fowler
alijibu: “Bila shaka. Amewaangusha Watu wengi sana, ikiwa pamoja na
yeye!”
Fowler, ambae alifunga Bao 183 katika
Mechi 369 kwa Liverpool, amesema: "Klabu ilikuwa upande wake na
kumsapoti, pia Masapota, na hii ni kwa sababu ni Mchezaji mzuri mno.
Ndio alisinikiza kuhama lakini bado yupo Liverpool. Sidhani kama atapata
nafasi nyingi akileta upumbavu wake Uwanjani!”
Suarez alihamia Liverpool kutoka Ajax
Januari 2011 lakini tangu wakati huo amekumbwa na utata mkubwa Uwanjani
na kufungiwa mara kadhaa na kutwangwa Faini.
+++++++++++++++++++++++++++++++
PATA MATUKIO YA UTATA YA SUAREZ KATIKA ULIMWENGU WA SOKA:
Novemba 2007
Akiwa Nahodha wa Ajax alifungiwa na Klabu yake baada ya kupigana na mwenzake Albert Luque wakati wa Haftaimu kwenye Mechi.
Julai 2010
Afrika na Dunia nzima itamkumbuka
Suarez, ambae ni Mchezaji wa Uruguay, kwa kuikatili Ghana huko Afrika
Kusini kwenye mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Dunia alipoushika mpira
kwa makusudi kwenye mstari wa goli dakika ya mwisho ya muda wa nyongeza
na kuwanyima Ghana goli la wazi la ushindi.
Kwa kitendo hicho, Suarez aliwashwa Kadi
Nyekundu na Ghana kupewa penati lakini Asamoah Gyan, ambae aliwahi kuwa
Ligi Kuu England na Timu ya Sunderland, alikosa kufunga penati hiyo.
Novemba 2010
Alipata Kifungo cha Mechi 7 akiwa huko
Uholanzi na Klabu ya Ajax baada ya kumng’ata meno Mchezaji wa PSV
Eindhoven Otman Bakkal kwenye mechi ya Ligi huko Uholanzi.
Octoba 2011
Wakicheza na Everton, alivunga amechezewa faulo na Jack Rodwell na kujidondosha na Rodwell akapewa Kadi Nyekundu.
Octoba 2011
Suárez alimkashifu Kibaguzi Patrice Evra wa Manchester United na kufungiwa Mechi 7 na kupigwa Faini Pauni 40,000.
Decemba 2011
Akiwa kwenye mashitaka ya kumkashifu
Kibaguzi Patrice Evra wa Manchester United na kabla hajahukumiwa
alionekana kutoa ishara ya matusi kwa Mashabiki wa Fulham kitendo
ambacho kilimpa Kifungo cha Mechi 1.
Februari 2012
Man United na Liverpool walikutana tena
Old Trafford kwa mara ya kwanza tangu tukio la Suarez kumkashifu
Kibaguzi Evra na Suarez, bila kutarajiwa, aligoma kumpa mkono Evra.
Octoba 2012
Alishangilia Goli lake kwa kujirusha
mbele ya Meneja wa Everton, David Moyes, ambae kabla ya Mechi hiyo na
Liverpool alitamka Wachezaji wadanganyifu kama Suarez wnaohadaa Marefa
wanafanya Mashabiki waikatae Soka ya England.
Januari 2013
Alipoza mpira kwa mkono na kufunga Bao
la ushindi kwa Liverpool kwenye Mechi ya Raundi ya 3 ya FA CUP dhidi ya
Timu ya Daraja la chini Mansfield.
Machi 2013
Akiichezea Nchi yake Uruguay kwenye
Mechi ya Mchujo ya kuwania kuingia Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil
Mwaka 2014, Suarez alionekana kumtandika ngumi Beki wa Chile Gonzalo
Jara bila Refa kuona.
FIFA walichunguza tukio hili na kutochukua hatua yeyote.
+++++++++++++++++++++++++++++++
Robbie Fowler amemtaka Suarez kuonyesha
uaminifu wake kwa Liverpool pale aliposema : “Wapo Wachezaji wanaofanya
vitu vya kipumbavu na kijinga, si sawa lakini unategemea uaminifu toka
kwao. Usiruhusu Watu wakunyooshee kidole nenda Uwanjani fanya Vitu
sahihi na uwe Mchezaji mwenye Kipaji ambacho tunajua unacho! Sasa tuanze
kuongea kuhusu Suarez Mchezaji Bora na si Mchezaji anaefanya upumbavu
Uwanjani!”
TATHMINI>>CAPITAL ONE CUP-Raundi ya Tatu: Man United v Liverpool
UWANJA: Old Trafford
SIKU: Jumatano Septemba 25 SAA: 3 Dak 45 Usiku

STAA wa Manchester United Robin van
Persie huenda asicheze Mechi hii kwani anasumbuliwa na Nyonga
iliyomfanya pia aikose Mechi ya Jumapili iliyopita na Man City.
Pia, Mabeki wa Man United, Rafael na
Phil Jones, wapo kwenye hatihati lakini upo uwezekano wa Mawinga Nani na
Wilfried Zaha kucheza.
Fowadi wa Liverpool Luis Suarez yupo huru kucheza baada ya kumaliza Kifungo cha Mechi 10.
Liverpool huenda ikamkosa Beki Daniel
Agger mwenye tatizo la mbavu lakini Glen Johnson, Philippe Coutinho na
Joe Allen ni majeruhi.
Tathmini
Kawaida Mechi za Kombe la Ligi, ndio
hili Capital One Cup, Klabu huchezesha Wachezaji Chipukizi na wale ambao
hawana Namba za kudumu kwenye Kikosi cha Kwanza lakini hii ni Bigi
Gemu, Manchester United v Liverpool, na ndio Mechi ya kwanza tu tokea
Man United wafungwe na Mahasimu wao wengine Man City na pia hii ni
nafasi ya kwanza kwa Luis Suarez kuichezea Liverpool tokea Aprili baada
ya kuwa Kifungoni, hivyo tegemea Wachezaji Mastaa na ‘fulu nondo’ toka
kila Timu.
Uso kwa Uso
-Kwenye Kombe la Ligi, Manchester United
na Liverpool zimekutana mara 4 na Liverpool kushinda Fainali za 1983 na
2003 na pia Mechi ya Raundi ya Nne Mwaka 1985 huko Anfield huku Man
United wakishinda Mechi ya Raundi ya Tatu Uwanjani Old Trafford Mawaka
1991.
-Uwanjani Old Trafford, Man United
wameishinda Liverpool mara zote 5 katika Mechi zote 5 zilizochezwa
mwisho Uwanjani Old Trafford.
-Mara ya mwisho kwa Man United kufungwa na Liverpool Old Trafford ni Machi 2009 walipofungwa Bao 4-1 kwenye Mechi ya Ligi.
REKODI: USO KWA USO
MAN UNITED USHINDI |
SARE
|
LIVERPOOL USHINDI
|
|
LIGI
|
63
|
44
|
54
|
FA CUP
|
9
|
4
|
4
|
LIGI CUP
|
1
|
0
|
3
|
NYINGINE
|
1
|
3
|
2
|
JUMLA
|
74
|
51
|
63
|
0 comments:
Post a Comment