Kama vipi mpeni Wenger Kagawa muone
MANCHESTER, ENGLAND
ASIA nzima ilisubiri kumtazama Shinji Kagawa akicheza Anfield, lakini dah! haikuwa hivyo.
Wamekerwa wengi, Wajerumani wa Borussia Dortmund na hata wapenzi wa kuwatuza viungo waongo waongo ndani ya uwanja.
‘Free Shinji’, kampeni hii ya mashabiki wa
Dortmund na Wahispania inafahamu uwezo wa miguu wa Mjapani huyo na kile
Manchester United inachomfanyia. Borussia Dortmund wanamtaka mtu wao.
Kuna tofauti kubwa kati ya Manchester United na
klabu nyingine linapokuja suala la sifa za nje ya uwanja. Wakati Kagawa
alipowekwa benchi nchini Ujerumani, nje ya Ruhr na Japan, ni watu
wachache walilitambua hilo.
Lakini, akikaa benchi Old Trafford, dunia nzima
inatambua. Hasa kwa mchezaji wa kiwango na kipaji kama chake, hilo
litawagusa wengi, ukizingatia staili ya uchezaji wa Manchester United
inahitaji mtu kama yeye ndani ya uwanja.
Alipokaa benchi dhidi ya Swansea ilieleweka
kwasababu staa huyo alikuwa kwenye mechi ya kimataifa ya Japan katikati
ya wiki, lakini aliposugua pia kwenye mechi dhidi ya Chelsea, hilo
limeumiza watu.
Kuna wanaosema kwamba bado hayupo kwenye kiwango
bora, lakini kwenye kikosi cha Japan alicheza kwa dakika zote 90 na
kufunga katika mechi dhidi ya Uruguay.
Hivyo basi, hata kama hakuwa fiti kwa dakika zote,
bado alipaswa kucheza walao kwa dakika 15 hadi 20 kwenye mechi hiyo ya
Chelsea, kitu ambacho hakikutokea.
Kocha wa Borussia Dortmund, Jurgen Klopp, amesema
Kagawa ni kati ya wachezaji bora duniani, hivyo yanamtoka machozi kuona
anabwagwa benchi.
Mashabiki kutoka sehemu mbalimbali duniani
waliguswa kuona mchezaji huyo amekosa nafasi ya kucheza kwenye mchezo
dhidi ya Chelsea.
Aliwekwa kando si tu mwanzoni mwa mchezo, hata
Manchester United ilipofanya mabadiliko, ilichagua kuwaingiza Ashley
Young na Ryan Giggs, yeye akiendelea kubaki benchi.
0 comments:
Post a Comment