Taarifa
za mwanzo za kusikitisha ambazo tumezipata hivi punde zinasema mtu
mmoja anayedhaniwa kuwa mume au mchumba wa mwandishi wa habari wa ITV na
Radio One Ufoo Saro amefanya mauaji ya kutisha na yeye mwenyewe kujiua.
Akizungumza na radio one kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni kamanda Wambura amesema tukio hilo limetokea majira ya alfajiri ya leo.
Kamanda wambura ameongeza kuwa mwanaume huyo anafanya kazi Umoja wa Mataifa (UN) huko Sudani
ila bado haijafahamika kwamba anafanyia kitengo gani (japo kwa habari
za mtaani zinasema mtu huyo ni mwanajeshi ila bado hazijathibitishwa)
Kamanda
Wambura anasema inasemekana kulikua kuna ugomvi kati ya wawili hao
ambapo walishindwa kuelewana na ndipo walipoamua kwenda kwa mama mzazi
wa Ufoo Saro (mama mkwe) na ndipo mwanaume huyo alipomshutumu mama mkwe
wake kwamba anamtetea mwanae ndipo alipotoa bastola na kumpiga mama yake
na Ufoo Saro Risasi ya kichwa na kumuua papo hapo na kisha akampiga
Ufoo Saro risasi ya mbili moja ya tumboni na ingine ya mguuni na kudhani
kwamba amemuua kumbe amemjeruhi tu kisha kujipiga mwenyewe risasi ya
kidevuni na kufariki dunia hapo hapo.
TAARIFA ZAIDI NA PICHA ZA TUKIO ZITAKUJA PUNDE HAPA HAPA MTANDAO WA UHAKIKA
0 comments:
Post a Comment