MANCHESTER CITY YAIFUNGA NEWCASTLE 4-0, CITY WAANZA MSIMU MPYA KWA KUGAWA KICHAPO MBELE YA KOCHA WAO MPYA PELEGRINI YATOA VITISHO KWA MANCHESTER UNITED, ARSENAL, CHELSEA.
Ligi kuu ya nchini Uingereza
imeendelea tena leo hii usiku Machester City na Newcastle United, Kocha Manuel
Pellegrini wa City akishuhudia timu yake ikitoa kibano cha uhakika na kutimiza
yale aliyokuwa akijigamba nayo kuwa anakikosi safi, Yakionekana wazi baada ya
wachezaji wake kuifunga bao nne, mbili zikipatikana kipindi cha kwanza na mbili
kipindi cha pili kwa timu ya Newcastle inayoongozwa na kocha Alan Pardew usiku
huu.
Bao la kwanza likifungwa
na Silva dakika ya 6, huku mchezaji
matata Aguero akimalizia bao la pili dakika ya 22 dhidi ya Newcastle, huku
Newcastle wakiambulia mwenzao Taylor akipewa
kadi nyekundu baada ya kumfanyia ndivyo sivyo Sergio Aguero huku akiwa na kadi ya njano aliyopewa mapema katika
kipindi hiki cha kwanza. Kipindi cha pili pia hakikupishana sana na kipindi cha
kwanza City wameanza na machachali sana na kufanikiwa kupata bao la tatu kupitia
mchezaji Toure kwa kupiga frii kiki
kuelekea golini dakika ya 50.
Dakika ya 75 mchezaji Nasri akipewa pasi safi
akawachomoka mabeki wa Newcastle na kuipachikia bao la nne City na kufanya 4-0
dhidi ya timu ya Newcastle.Manchester City kipindi hiki cha pili pia wametumia
mwanya wa wachezaji pungufu wa Newcastle na kuutumia vizuri huku wakiwashambulia
na kufika mara nyingi kwenye lango la Newcastle.
Sergio Aguero akichonga ...hapa na kutupia!!
David Silva ndiye aliyeanza kufunga bao
Silva akishangilia baada ya kufunga!!
Aguero cakishangilia baada ya kufunga bao..
Mchezaji Steven Taylor akifanyia majanga mchezaji wa City
Sergio Aguero hapa na kupewa kadi nyekundu.
Refa Andre Marriner Steven Taylor akimwonesha kadi
nyekundu
Toure akishangilia kimya kimya baada ya kuifunga timu ya
Newcastle bao la tatu.
Kocha Manuel Pellegrini akiongea na Samir Nasri kabla ya
kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya Sergio Aguero.
Samir Nasri akifunga bao la mwisho na kufanya 4-0 dhidi ya
Newcasle
Nasri akishangilia baada ya kufunga bao la 4
VIKOSI:
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Lescott, Clichy, Fernandinho, Toure, Jesus Navas, Aguero (Nasri 61), Silva, Dzeko.
Subs: Milner, Negredo, Kolarov, Javi Garcia, Rodwell, Pantilimon.
Booked: Dzeko, Fernandinho.
Goals: Silva 6, Aguero 22, Toure 50, Nasri 75.
Newcastle United: Krul, Debuchy, Coloccini, Steven Taylor, Yanga-Mbiwa, Sissoko, Tiote, Gouffran (Dummett 45+4), Ben Arfa, Gutierrez (Anita 44), Cisse.
Subs: Elliot, Marveaux, Shola Ameobi, Obertan, Sammy Ameobi.
Booked: Yanga-Mbiwa, Sissoko, Debuchy.
Sent off: Taylor.
Referee: Andre Marriner (W Midlands)

VIKOSI:
Manchester City: Hart, Zabaleta, Kompany, Lescott, Clichy, Fernandinho, Toure, Jesus Navas, Aguero (Nasri 61), Silva, Dzeko.
Subs: Milner, Negredo, Kolarov, Javi Garcia, Rodwell, Pantilimon.
Booked: Dzeko, Fernandinho.
Goals: Silva 6, Aguero 22, Toure 50, Nasri 75.
Newcastle United: Krul, Debuchy, Coloccini, Steven Taylor, Yanga-Mbiwa, Sissoko, Tiote, Gouffran (Dummett 45+4), Ben Arfa, Gutierrez (Anita 44), Cisse.
Subs: Elliot, Marveaux, Shola Ameobi, Obertan, Sammy Ameobi.
Booked: Yanga-Mbiwa, Sissoko, Debuchy.
Sent off: Taylor.
Referee: Andre Marriner (W Midlands)
0 comments:
Post a Comment