Connection

Services

Computer Maintanance

Computer Supply

Laptop Repair

Networking Installation



Learn more

Tuesday, 20 August 2013

Filled Under:

UDAKU

Share

HUYU NDO MFANYABIASHARA ANAYEWALAWITI WATOTO KWA KUWAPAKA MAFUTA KISHA KUANZA KUFANYA NAO MAPENZI

Stori:Mwandishi wetu, Mbeya
Inasikitisha sana! Erasto Mwakyoma (50), mkazi wa Mtaa wa Mapelele, Kata ya Ilemi jijini hapa anashikiliwa na Jeshi la Polisi Kituo Kuu kwa tuhuma za ulawiti wa watoto wawili wa kike, mmoja mwenye umri wa miaka minne na mwingine mitano na kusababisha wakazi wake kuangua vilio.
Mtuhumiwa
Habari zilidai kuwa katika tukio hilo,  wazazi wa watoto hao walipokea malalamiko kutoka kwa watendewa hao wakidai kuingiliwa na mfanyabiashara huyo wa duka.
Ilielezwa kuwa baada ya wazazi kupata malalamiko hayo, walitoa taarifa kwa Balozi wa Mtaa, Casian Mwezimpya ambaye aliamua kulipeleka suala hilo kwa Mwenyekiti wa Mtaa, Christopher Mwakibete.
Watoto waliolawitiwa
Baada ya msala kutua mezani kwake huku wananchi wakitaka kumtoa roho, mwenyekiti huyo aliamua kuwaita wazazi na mtuhumiwa kisha kuwahoji ambapo watoto hao walipewa nafasi ya kueleza kila kitu.
Mwenyekiti wa Serikali za miitaa akiandika maelezo
Watoto hao walieleza kuwa mwanaume huyo alikuwa akiwashika sehemu za siri na kuwapaka mafuta kisha kufanya nao mapenzi.
Baada ya kuwasikiliza kwa makini, Mwakibete aliona suala hilo ni maji marefu kwake kwa kuwa ni la kisheria na kitaalamu hivyo alilazimika kulipeleka polisi.
Wakati Mwakibete akiwa kwenye harakati hizo, mwenyekiti wa dawati la watoto mtaa huo, Mary Gumbo aliingilia kati na kumchukua mtuhumiwa huyo hadi Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapa.
Ilifahamika kuwa wakati mahojiano ya awali kati ya mtuhumiwa na polisi yakiendelea, Mary aliwachukua watoto hadi Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa uchunguzi na mtuhumiwa kubaki kituoni hapo kwa mahojiano zaidi na hatua za kisheria.
Hata hivyo, uchunguzi ulibaini kuwa baadhi ya watoto wa mtaa huo wamekuwa wakitendewa vitendo vya ukatili lakini vimekuwa vikifumbiwa macho na baadhi ya wazazi wakiamini ni aibu kwa watoto wao.

0 comments:

Post a Comment

2014 © Movieism
RealMag theme by Templateism