Connection

Services

Computer Maintanance

Computer Supply

Laptop Repair

Networking Installation



Learn more

Thursday, 26 September 2013

Filled Under:

MICHEZO

Share

CAPITAL ONE CUP: MAN UNITED USHINDI DHIDI LIVERPOOL , ARSENAL MATUTA!

>>MABINGWA SWANSEA NJE!!
>>DROO RAUNDI YA 4: ARSENAL v CHELSEA, MAN UNITED v NORWICH CITY!

CAPITAL ONE CUP Jana Usiku ilimaliza Raundi ya Tatu kwa Mabingwa wa England, Manchester United, kuibwagaCAPITAL_ONE_CUP-BEST Liverpool Bao 1-0 na Arsenal kwenda Dakika 120 na WBA na kusonga kwa Penati huku Mabingwa Watetezi, Swansea City, wakibwagwa nje na Timu ya Daraja la chini, Birmigham City.
++++++++++++++++++++++++++++
CAPITAL ONE CUP
RAUNDI YA TATU
MATOKEO:
Jumatano Septemba 25
Birmingham 3 Swansea 1
Manchester United 1 Liverpool 0
Newcastle 2 Leeds 0
Tranmere 0 Stoke 2
West Brom 1 Arsenal 1 [Arsenal Penati 4-3]
++++++++++++++++++++++++++++
DROO YA RAUNDI YA 4:
Sunderland v Southampton
Leicester City v Fulham
Birmingham City v Stoke City
Manchester United v Norwich City
Burnley v West Ham United
Arsenal v Chelsea
Tottenham Hotspur v Hull City
Newcastle United v Manchester City
**Mechi kuchezwa Wiki ya kuanzia Oktoba 28
++++++++++++++++++++++++++++
MAN UNITED 1 LIVERPOOL 0
Javier Hernandez ‘’Chicharito’  ameipeleka Manchester United Raundi ya Nne ya Capital One Cup baada ya kufunga Bao pekee Sekunde ya 39 tu tangu Kipindi cha Pili kianze alipounganisha Kona ya Wayne Rooney na kuwabwaga Liverpool kwa Bao 1-0.
Rooney ndie alikuwa Nahodha wa Kikosi kilichobadilishwa Wachezaji wanane toka kile kilichobondwa 4-1 na Man City Jumapili iliyopita huku Liverpool wakiwa na Kikosi chao kamili pamoja na Luis Suarez, Straika wao aliekuwa Kifungoni kwa Mechi 10, ambae alianza Mechi hii baada kumaliza Kifungo chake.
VIKOSI:
Man United: De Gea; Rafael, Smalling, Evans, Buttner; Nani, Jones, Giggs, Kagawa, Nani; Hernandez, Rooney
Akiba: Anderson, Carrick, Welbeck, Fabio Da Silva, Zaha, Amos, Januzaj.
Liverpool: Mignolet; Sakho, Touré, Skrtel, Enrique; Henderson, Lucas, Gerrard; Moses, Suarez, Sturridge
Akiba: Brad Jones, Alberto, Aspas, Sterling, Ibe, Kelly, Wisdom
Refa: M Clattenberg
BIRMINGHAM 3 SWANSEA 1
Mabingwa Watetezi wa Kombe hili, Swansea City, wamepigwa mweleka na Klabu ya Daraja la chini la Championship, Birmingham City, kwa kutandikwa Bao 3-1.
Bao za Birmingham zilifungwa na Burn, Dakika ya 57, Green, 61 na Adeyemi, 81.
Bao la Swansea lilifungwa na Bony katika Dakika ya 90.
VIKOSI:
Birmingham: Doyle, Spector, Burn, Robinson, Reilly, Caddis, Adeyemi, Hancox, Burke, Green, Ferguson
Akiba: Ambrose, Lovenkrands, Arthur, Lee, Shinnie, Allan, Townsend.
Swansea: Tremmel, Tiendalli, Amat, Monk, Taylor, Lamah, de Guzman, Britton, Pozuelo, Shelvey, Bony
Akiba: Vorm, Chico, Michu, Routledge, Canas, Vazquez, Ben Davies.
Refa: Keith Stroud
TRANMERE 0 STOKE 2
Bao mbili za Stephen Ireland na Peter Crouch ziliwapa ushindi wa Ugenini Stoke City walipoibwaga Timu ya Daraja la Chini Tranmere Rovers.
VIKOSI:
Tranmere: Fon Williams, Hateley, Dugdale, Taylor, Horwood, Rowe, Atkinson, Power, Akpa Akpro, Lowe, Stockton
Akiba: Holmes, Goodison, Thompson, Bell-Baggie, Sodje, Davies, Mooney.
Stoke: Sorensen, Cameron, Huth, Shawcross, Muniesa, Whelan, Palacios, Ireland, Pennant, Crouch, Arnautovic
Akiba: Jones, Adam, Walters, Butland, Assaidi, Etherington, Wilkinson.
Refa: David Coote
NEWCASTLE 2 LEEDS 0
Newcastle wamesonga mbele kwa ushindi wa Bao 2-0 dhidi ya Leeds United na Bao zao zilifungwa na Papiss Cisse na Yoan Gouffran.
VIKOSI:
Newcastle: Krul, Debuchy, Williamson, Coloccini, Dummett, Gouffran, Anita, Tiote, Marveaux, Sammy Ameobi, Cisse
Akiba: Ben Arfa, Yanga-Mbiwa, Gosling, Bigirimana, Obertan, Vuckic, Alnwick.
Leeds: Kenny, Byram, Wootton, Pearce, Warnock, Austin, Mowatt, Tonge, McCormack, Smith, Poleon
Akiba: Murphy, Green, Hunt, White, Brown, Diouf, Cairns.
Refa: Mike Jones
WEST BROM 1 ARSENAL 1
Dakika 90 za Mchezo matokeo yalikuwa Bao 1-1 kwa Bao za Thomas Eisfeld kwa Arsenal katika Dakika ya 61 na Saido Berahino kuisawazishia WBA katika Dakika ya 71 na Dakika za Nyongeza zikabaki hivyo hivyo na Arsenal kusonga kwa Penati 4-3.
VIKOSI:
West Brom: Luke Daniels, Reid, Lugano, Dawson, Popov, Sessegnon, Mulumbu, Dorrans, Sinclair, Berahino, Long
Akiba: Olsson, Morrison, Rosenberg, Camp, Amalfitano, McAuley, Billy Jones.
Arsenal: Fabianski, Jenkinson, Mertesacker, Vermaelen, Monreal, Miyaichi, Hayden, Arteta, Gnabry, Eisfeld, Bendtner
Akiba: Flamini, Park, Akpom, Bellerin, Olsson, Iwobi, Viviano.
Refa: Robert Madley
++++++++++++++++++++++++++++
DONDOO MUHIMU:
-KLABU 92 za BPL [Klabu 20] na Ligi za Madaraja Matatu ya chini [Championship, Ligi 1 na 2, Jumla Klabu 24 kila Ligi] hushiriki Raundi 7 za Mashindano.
-NUSU FAINALI huchezwa kwa Mtindo wa Mtoano wa Nyumbani na Ugenini.
-KLABU ZA BPL HUANZA kushiriki Raundi ya Pili lakini zile ambazo zinacheza Mashindano ya UEFA ya CHAMPIONZ LIGI na EUROPA LIGI huanza kucheza Raundi ya Tatu.
-FAINALI ITACHEZWA TAREHE 2 MACHI 2014 Uwanja wa Wembley na Bingwa hushiriki UEFA EUROPA LIGI Msimu unaofuata.
-MFUMO:
Raundi ya 1: Wiki ya kuanzia Agosti 5
Raundi ya 2: Wiki ya kuanzia Agosti 26
Raundi ya 3: Wiki ya kuanzia Septemba 23
Raundi ya 4: Wiki ya kuanzia Oktoba 28
Raundi ya 5: Wiki ya kuanzia Desemba 16
Nusu Fainali-Mechi ya Kwanza: Wiki ya kuanzia Januari 6
Nusu Fainali-Marudiano: Wiki ya kuanzia Januari 20
Fainali: Jumapili 2 Machi 2014

0 comments:

Post a Comment

2014 © Movieism
RealMag theme by Templateism