LEO SPURS v CHELSEA, BIFU AVB, MOURINHO LATOKOTA!!
>>AVB: ‘SPURS UPO UWEZO KUPIGANIA UBINGWA!’

Mbali ya upinzani ndani ya Uwanja ambapo
Tottenham wapo Nafasi ya Pili, Pointi sawa na Vinara Arsenal, na
Chelsea wako Nafasi ya 4, Pointi 2 nyuma ya Tottenham, nje ya Uwanja
Wiki hii yote Mechi hii imekolezwa na uhasama kati ya Mameneja wa Timu
hizi mbili ambao waliwahi kufanya
kazi pamoja kwa muda mrefu.

Kwa Kipindi cha Miaka 7, AVB na Mourinho
walikuwa Mtu na Msaidizi wake huko Klabu za FC Porto, Chelsea na Inter
Milan na ndipo wakatengana na Andre Villas-Boas kurudi FC Porto na
kutwaa Ubingwa na Kombe la Ureno pamoja na EUROPA LIGI katika Msimu
mmoja na kisha kuhamia Chelsea Mwaka 2011 kumrithi Carlo Ancelotti.
Majuzi, AVB alidokeza kuwa yeye na
Mourinho hawana uhusiano na hapotezi usingizi kwa kutengana kwao na
chanzo cha ugomvi wao ni Mourinho kumnyima nafasi ya kuwajibika zaidi
walipokuwa wote Inter Milan.
Nae Mourinho amejibu mapigo kwa kwa
kumsema AVB anakuwa kama ‘Mtoto’ kwa kuongea kwenye kadamnasi badala ya
kukutana uso kwa uso na kumaliza bifu lao.
SPURS NA UBINGWA
Wakati huo huo, Andre Villas-Boas
anaamini kuwa Tottenham sasa inao uwezo wa kupigania kunyakua Ubingwa
kwa vile Kikosi chao kimeimarika zaidi.
Baada kutumia Pauni Milioni 103 kabla
Msimu huu kuanza kwa kununua Wachezaji 7 wapya, Spurs imeshinda Mechi 8
kati ya 9 ilizocheza na sasa wako Nafasi ya Pili kwenye Ligi.
Tottenham hawajatwaa Ubingwa wa Daraja
la Juu England tangu Mwaka 1961 lakini Msimu huu, Meneja wa Tottenham,
AVB, anaamini mambo yanaweza kuwa tofauti.
Ametamka: “Inaonekana ni hivyo. Hakuna
Timu iliyonyakua Pointi zote kwenye Ligi. Mabingwa Man United
wanahangaika ingawa Ratiba yao ya mwanzo ni ngumu kupita Timu yeyote.
Man City wamefungwa Cardiff na kutoka Sare na Stoke. Sie Jumamosi
tunaweza kutoka tumefungwa Mechi mbili au Chelsea ikawa wao wamefungwa
Mechi mbili. Msimu huu unaonyesha kuwa hivyo, usiotabirika!”
Miongoni mwa Wachezaji wao wapya,
Roberto Soldado amefunga Bao 4 katika Mechi 6, Paulinho na Christian
Eriksen wametamba kwenye Kiungo.
Kuimarika kwa Kikosi cha Tottenham
kulidhihirika Jumanne iliyopita kwenye Capital One Cup ambapo Timu
iliyobadilishwa Wachezaji 8 iliinyuka Aston Villa Bao 4-0 tena Ugenini
huku Mkongwe wao Jermaine Defoe akiwa Nyota kwa kupiga Bao 2.
Ingawa Kikosi kinaonekana kimeimarika,
Spurs inao Mastraika wakubwa wawili tu, Defoe na Soldado, na imebidi
wamrudishe tena Emmanuel Adebayor kwenye Kikosi cha Kwanza baada ya
kutupwa kwenye Kikosi cha Akiba kufuatia kutokuwepo Mazoezini baada
kukumbwa na matatizo ya kibinafsi huko kwao Togo.
++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
BPL: LIGI KUU ENGLAND
Jumamosi 28 Septemba
14:45 Tottenham Hotspur v Chelsea
17:00 Aston Villa v Manchester City
17:00 Fulham v Cardiff City
17:00 Hull City v West Ham United
17:00 Manchester United v West Bromwich Albion
17:00 Southampton v Crystal Palace
19:30 Swansea City v Arsenal
Jumapili 29 Septemba
15:30 Stoke City v Norwich City
18:00 Sunderland v Liverpool
Jumatatu 30 Septemba
22:00 Everton v Newcastle United
0 comments:
Post a Comment