Connection

Services

Computer Maintanance

Computer Supply

Laptop Repair

Networking Installation



Learn more

Tuesday, 1 October 2013

Filled Under:

MICHEZO

Share

SHAKHTAR DONETSK v MAN UNITED, NI HEKAHEKA!!

>>KOCHA MIRCEA LUCESCU: ‘MOYES ANAATHIRIKA KWA KUBADILISHA TIMU SANA!’
SHAKHTAR_DONETSK_v_MAN_UNITEDWAKATI Shakhtar Donetsk inajiandaa kuikaribisha Manchester United ndani ya Donbass Arena huko Donetsk, Ukraine Jumatano Usiku kwenye Mechi yao ya Kundi A la UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, Kocha wao Mircea Lucescu amedai Man United inaathirika na kupata matokeo mabaya kwa vile Kocha wao David Moyes anabadilisha Kikosi chake kila Mechi.
Hii ni Mechi ya pili kwa kila Timu kwenye Kundi A na Shakhtar Donetsk ilianza vyema kwa ushindi wa Ugenini wa Bao 2-0 dhidi ya Real Sociedad na Man United kuichapa Bayer Leverkusen Bao 4-2 Uwanjani Old Trafford.
Wakati kwa David Moyes hii ni mara ya pili kuongoza Timu kwenye UCL, na ikiwa ni Mechi ya pili tu kwake na Man United, Lucescu anaongoza Kikosi kwa mara ya 109 kwenye Mechi za UCL na pia alikuwepo kama Meneja kwenye Timu ya Inter Milan ya Mwaka 1999 iliyotolewa na Man United kwenye UCL na Man United kutinga Fainali na kuichakaza Bayern Munich na kuwa Bingwa.
Siku 3 baada ya Mechi hiyo ya Robo Fainali huko San Siro  ambayo Inter Mian waliongoza kwa Bao 1 na Man United kurudisha na hatimae kutinga Fainali, Mircea Lucescu alijiuzulu Umeneja Inter Milan.
Lucescu, Kocha Mkongwe mwenye Miaka 68, ameeleza: “Kila Kocha mpya anakuja na falsafa yake na inachukua muda. Lakini tumechunguza Gemu za United na tumeona kila Mechi anabadili Wachezaji labda wanne au watano. Ubadilishaji huu unasababisha Wachezaji kupoteana.Tumeona Klabu nyingine kubwa huko England Chelsea, Liverpool na Arsenal hawabadili sana na pengine hii ndio sababu hawafanyi vizuri.”

TATHMINI YA MECHI:
>>DONBASS ARENA, DONETSK, UKRAINE JUMATANO SAA 03:34 USIKU
Man United wanaingia kwenye Mechi hii wakitokea kwenye Wiki ngumu ambayo walifungwa 4-1 na Man City kwenye Ligi, kuifunga Liverpool 1-0 kwenye Capital One Cup na kufungwa 2-1 na West Brom kwenye Ligi.
Shakhtar Donetsk wao Jumamosi iliyopita walitoka nyuma 2-0 na kutoka Sare 2-2 na Wapinzani wao wakubwa wa Mjini Donetsk, Metallurg Donetsk, kwenye Mechi ya Ligi Kuu ya Ukraine.
Man United na Shakhtar Donetsk hazijawahi kukutana lakini Man United wameshacheza na Klabu ya Ukraine Dynamo Kiev mara 4 na kushinda mara 3 na sare 1.
Shakhtar imesheheni Wachezaji toka Brazil na Kiungo Alex Teixeira ndie Nyota ambae pia ndie aliefunga Bao zote 2 walipoitwanga Real Sociedad Bao 2-0 kwenye Mechi ya kwanza ya Kundi hili.

VIKOSI:
MANCHESTER UNITED:
MENEJA: David Moyes
MAKIPA: 1. David De Gea, 13, Anders Lindegaard, 50. Sam Johnstone;
MABEKI: 2. Rafael da Silva, 3. Patrice Evra, 4. Phil Jones,  6. Jonny Evans, 12. Chris Smalling, 15. Nemanja Vidic, 28. Alexander Büttner, 39. Tom Thorpe;
VIUNGO: 8. Anderson, 11. Ryan Giggs, 16. Michael Carrick, 17. Nani, 18. Ashley Young, 23. Tom Cleverley, 25. Antonio Valencia, 26. Shinji Kagawa, 31. Marouane Fellaini,
MASTRAIKA: 10. Wayne Rooney, 14. Javier Hernandez, 19. Danny Welbeck, 20. Robin van Persie,

SHAKHTAR DONETSK:
MENEJA: Mircea Lucescu
MAKIPA: 30. Andriy Pyatov, 32. Anton Kanibolotskiy, 35. Mykyta Kriukov;
MABEKI: 4. Olexandr Volovyk, 5. Olexandr Kucher, 13. Vyacheslav Shevchuk, 27. Dmytro Chygrynskiy, 38. Serhiy Kryvtsov, 44. Yaroslav Rakitskiy;
VIUNGO: 3. Tomáš Hübschman, 6. Taras Stepanenko, 8. Fred, 10. Bernard, 14. Vasyl Kobin, 17. Fernando, 20. Douglas Costa, 24. Dmytro Grechyshkin, 29. Alex Teixeira, 33. Darijo Srna, 77. Ilsinho;
MASTRAIKA: 9. Luiz Adriano, 11. Eduardo, 19. Facundo Ferreyra, 28. Taison
REFA: Pavel Kralovec [Czech Republic]

RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumatano 2 Oktoba 2013
[Saa 1 Usiku]
PFC CSKA Moskva v FC Viktoria Plzeň
[Zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku]
FC Shakhtar Donetsk v Manchester United FC
Bayer 04 Leverkusen v Real Sociedad de Fútbol
Juventus v Galatasaray A.Ş.
Real Madrid CF FC København
Paris Saint-Germain v SL Benfica
RSC Anderlecht v Olympiacos FC
Manchester City FC v FC Bayern München

0 comments:

Post a Comment

2014 © Movieism
RealMag theme by Templateism