ARSENAL WAPIGA, CHELSEA & DORTMUND WABAMIZA, BARCA WATUNGUA!!
>>JUMATANO: MAN UNITED WAPO UKRAINE, CITY v BAYERN!!
Mechi za pili za Makundi E hadi H za
UEFA CHAMPIONZ LIGI zimechezwa Usiku huu na Timu za England, Arsenal na
Chelsea, zimefanya vyema kwa kupata ushindi mnono.
PATA RIPOTI KAMILI:
+++++++++++++++++++++++++++++++
MATOKEO:
Jumanne 1 Oktoba 2013
Football Club Zenit 0 FK Austria Wien 0
FC Basel 0 FC Schalke 1
FC Steaua Bucureşti 0 Chelsea 4
Borussia Dortmund 3 Olympique de Marseille 0
Arsenal 2 SSC Napoli 0
FC Porto Club 1 Atlético de Madrid 2
AFC Ajax 1 AC Milan 1
Celtic 0 FC Barcelona 1
+++++++++++++++++++++++++++++++

KUNDI E
BASEL 0 SCHALKE 1
FC Basel, ambao walianza Kundi E kwa
kishindo kwa kuichapa Chelsea Bao 2-1 huko Stamford Bridge, leo wakiwa
kwao wametunguliwa Bao 1-0 na Schalke.
Bao la ushindi kwa Schalke lilifungwa na Draxler katika Dakika ya 54.
STEAUA BUCHAREST 0 CHELSEA 4
Chelsea leo wamezinduka Ugenini kwa
kuitwanga Steau Bucharest Bao 4-0 kufuatia kupoteza Mechi ya kwanza ya
Kundi E walipofungwa 2-1 na Basel.
Bao za Chelsea zilipachikwa na Ramires
Dakika za 19 na 55, Georgievski aliejifunga mwenyewe katika Dakika ya 44
katika harakati za kuokoa shuti la Samuel Eto’o lililotemwa na Kipa na
Bao la 4 kufungwa na Frank Lampard katika Dakika ya 90.
VIKOSI:
Steaua București: Tatarusanu; Georgievski, Szukala, Gardos, Latovlevici; Filip, Bourceanu; Popa, Stanciu, Tanase, Piovaccari
Akiba: Nita, Prepelita, Cristea, Tatu, Neagu, Varela, Kapetanos
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cole, Luiz, Ramires, Lampard, Torres, Mata, Oscar, Schurrle, Terry
Akiba: Schwarzer, Mikel, Ba, Willian, Cahill, Azpilicueta, Eto'o
KUNDI F
BORUSSIA DORTMUND 3 MARSEILLE 0
Baada ya kuchapwa na Napoli Bao 2-1
katika Mechi yao ya kwanza, Borussia Dortmund Usiku huu wakicheza
Nyumbani waliitwanga Marseille Bao 3-0.
Bao za Dortmund zilifungwa na Robert Lewandowski katika Dakika ya 19 na 80 kwa Penati na jingine Marco Reus katika Dakika ya 52.
ARSENAL 2 NAPOLI 0
Wakicheza kwao Uwanja wa Emirates,
Arsenal wameishinda Napoli Bao 2-0 na huu ni ushindi wao wa pili kwenye
Kundi F baada ya kuifunga Marseille Bao 2-1 katika Mechi ya kwanza .
Bao za Arsenal zilifungwa na Nyota wao Mesut Özil katika Dakika ya 8 na Olivier Giroud kwenye Dakika ya 15.
VIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Arteta, Flamini, Ramsey, Rosicky, Giroud, Ozil.
Akiba: Fabianski, Vermaelen, Wilshere, Monreal, Bendtner, Jenkinson, Gnabry.
Napoli: Reina, Mesto, Albiol, Britos, Zuniga, Behrami, Inler, Callejon, Hamsik, Insigne, Pandev.
Akiba: Rafael Cabral, Mertens, Dzemaili, Fernandez, Armero, Cannavaro, Zapata.
Refa: Milorad Mazic (Serbia)
KUNDI G
ZENIT SAINT PETERSBUG 0 AUSTRIA VIENNA 0
Zenit St Petersburg na Austria Vienna zimeambua Pointi zao za kwanza za Kundi G baada ya kutoka Sare ya 0-0 huko Urusi.
Zenit St Petersburg walikosa Bao kadhaa
kupitia Wachezaji wao Hulk na Aleksandr Kerzhakov na kupata pigo pale
katika Dakika ya 44 Mchezaji wao Alex Witsel alipotolewa kwa Kadi
Nyekundu baada ya Rafu kwa Florian Mader kosa ambalo lilionekana
halikustaili Kadi hiyo.
Katika Mechi zao za kwanza, Zenit ilifungwa 3-1 na Atletico Madrid huko Spain na Vieena kuchapwa 1-0 Nyumbani na FC Porto.
FC PORTO CLUB 1 ATLÉTICO DE MADRID 2
FC Porto wakicheza kwao huko Ureno
walitangulia kupata Bao moja na kujikuta wakifungwa Bao 2 na kupoteza
Mechi walipopigwa Bao 2-1 na Atletico Madrid.
Bao la Porto lilifungwa na Martinez
kwenye Dakika ya 16 na Atletico kupiga Bao zao kupitia Godin Dakika ya
58 na Turan Dakika ya 86.
KUNDI H
AJAX 1 AC MILAN 1
Ajax, wakicheza Nyumbani, walifunga Bao
katika Dakika ya 90 kufuatia Kona na Denswil kuunganisha kwa kichwa
lakini katika Dakika za Nyongeza, Dakika ya 94, AC Milan walipewa Penati
ya utata baada ya Refa Eriksson kutoka Sweden kuamua Van Der Hoorn
alimchezea Rafu Mario Balotelli na Balotelli mwenyewe akafunga Penati
hiyo na Mechi kumalizika Bao 1-1.
VIKOSI:
Ajax: Cillessen; Van
Rhijn, Moisander (Van Der Hoorn 78), Denswil, Blind; S De Jong, C
Poulsen, Duarte (Schone 59); De Sa (Andersen 64), Sigthorsson, Fischer
AC Milan: Abbiati; Abate, Mexes, Zapata, Constant; Poli (Emanuelson 84), De Jong, Muntari; Montolivo; Robinho (Matri 80), Balotelli
Refa: Eriksson (SWE)
CELTIC 0 BARCELONA 1
Bao la Dakika ya 75 na Cesc Fabregas
limewapa Barcelona ushindi wa Bao 1-0 huko Celtic Park walipocheza na
Celtic ambao kuanzia Dakika ya 59 walicheza Mtu 10 baada ya Nahodha wao
Scott Brown kupewa Kadi Nyekundu kwa Rafu dhidi ya Neymar ingawa marudio
yalionyesha Kadi hiyo haikustahili.
VIKOSI:
Celtic: Forster; Lustig, Ambrose, Van Dijk, Izaguirre; Matthews, Brown, Mulgrew, Samaras; Commons; Stokes
Akiba: Zaluska, Biton, Balde, Rogic, Pukki, Kayal, Forrest.
Barcelona team: Valdes, Alves, Bartra, Pique, Adriano, Sergio, Xavi, Iniesta, Neymar, Fabregas, Pedro
Akiba: Pinto, Montoya, Dos Santos, Song, Sergi Roberto, Alexis Sanchez, Tello.
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumatano 2 Oktoba 2013
[Saa 1 Usiku]
PFC CSKA Moskva v FC Viktoria Plzeň
[Zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku]
FC Shakhtar Donetsk v Manchester United FC
Bayer 04 Leverkusen v Real Sociedad de Fútbol
Juventus v Galatasaray A.Ş.
Real Madrid CF FC København
Paris Saint-Germain v SL Benfica
RSC Anderlecht v Olympiacos FC
Manchester City FC v FC Bayern München
+++++++++++++++++++++++++++++++
MATOKEO-Mechi za Kwanza:
Jumanne 17 Sep 2013
Manchester United FC 4 Bayer 04 Leverkusen 2
Real Sociedad de Fútbol 0 FC Shakhtar Donetsk 2
Galatasaray A.Ş. 1 Real Madrid CF 6
FC København 1 Juventus 1
SL Benfica 2 RSC Anderlecht 0
Olympiacos FC 1 Paris Saint-Germain 4
FC Bayern München 3 PFC CSKA Moscow 0
FC Viktoria Plzeň 0 Manchester City FC 3
+++++++++++++++++++++++++++++
Jumatano 18 Sep 2013
FC Schalke 3 FC Steaua Bucureşti 0
Chelsea 1 FC Basel 2
Olympique de Marseille 1 Arsenal 2
SSC Napoli 2 Borussia Dortmund 1
FK Austria Wien 0 FC Porto 1
Club Atlético de Madrid 3 Football Club Zenit 1
AC Milan 2 Celtic FC 0
FC Barcelona 4 AFC Ajax 0
0 comments:
Post a Comment