MAJONZI MTANGAZAJI MKONGWE JULIAS NYAISANGA AFARIKI DUNIA
Habari mbaya na zenye kusikitisha ambazo
mtandao huu umezipata kutoka mkoani morogoro asubuhi hii ni kuwa
mtangazaji mkongwe hapa nchini Julius Nyaisanga maarufu kama "Uncle J"
(pichani) amefariki dunia
Kwa mujibu wa chanzo chetu taarifa za kifo chake zimezagaa asubuhi hii na bado haijafahamika zaidi sababu za kifo chake
Hadi Julius Nyaisanga anafariki dunia
alikuwa meneja wa kituo cha redio Abood FM cha mjini Morogoro, na
alijulikana sana tangu akifanya kazi Redio Tanzania sasa hivi
inajulikana kama TBC Taifa pia aliwahi kufanya kazi kituo cha ITV na Radio One stereo
Endelea kusoma blog hii tutakuletea taarifa zaidi za masiba huu mzito kwa jinsi tunavyozidi kuzipata
0 comments:
Post a Comment