Meneja wa Manchester United David Moyes amewaonya Wachezaji wake kuwa hatavumilia vitendo vya kujiangusha makusudi ili kuhadaa Marefaa kufuatia Ashley Young kupewa Kadi ya Njano kwenye Mechi ya ya Ligi Kuu England waliyoifunga Crystal Palace Bao 2-0
Katika Mechi hiyo Young alianguka ndani
ya boksi baada ya kupambana na Kagisho Dikgacoi katika Kipindi cha
Kwanza lakini marudio kwenye TV yalionyesha ni Young ndie aliemgonga
Mchezaji huyo kutoka Afrika Kusini.
Tukio hilo ndilo lilimpa Kadi Young
lakini baadae kwenye Kipindi hichi hicho Young aliangushwa na Dikgacoi
na Refa Jon Moss akaipa Man United Penati na kumpa Kadi Nyekundu
Dikgacoi kwa tukio hilo.
Na Moyes amesema: "Sitaki Wachezaji
wangu wajiangushe kuhadaa Marefa. Tukio la kwanza Dikgacoi alinyoosha
Mguu lakini Ashley aliusogeza Mguu wake ugongane."
Hata hivyo Moyes aliunga mkono uamuzi wa
kutoa Penati kwa tukio la pili kati ya Young na Dikgacoi lakini amesema
hapendezewi na Sheria ya kutoa Penati na Kadi Nyekundu kwa pamoja.
Nae
Meneja wa Crystal Palace, Ian Holloway, ambae Jana alikuwa akianza
kutumikia Kifungo chake cha Mechi mbili alichopewa baada ya kubatukia
Marefa katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi waliyocheza na Tottenham.
0 comments:
Post a Comment